IQNA

Washiriki katika mashindano ya Qur'ani ya wanachuo ni mabalozi wa Iran

12:24 - May 26, 2012
Habari ID: 2334117
Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 60 watakaoshiriki katika Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu watakaporejea katika nchi zao watakuwa kama mabalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Abbas Hashemi hafida wa Qur'ani Tukufu, akizungumza na IQNA kuhusu Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu amesema watakaoshiriki katika mashindano yao watabainisha kuhusu sura ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema kadiri kiwango cha mashindano hayo kinavyozidi kuimarika ndio yatakavyuo kuwa na taathira nzuri kwa washiriki. Ustadh Hashemi ambaye alichukua nafasi ya kwanza katika Mashindano ya KImataifa ya Qur'ani yaliyofanyika Tehran mwaka 2010 amesema maqari na mahufadh Wairani hujitaharisha vizuri kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
1016491
captcha