Wabunge hao walibeba mabango ya malalamiko na kusisitiza kwamba chama tawala kilifanya udanganyifu katika uchaguzi huo ili kuwapa ushindi wagombea wa chama hicho na kuwazuia wagombea wa Kiislamu kuingia bungeni kwa njia halali. Wengi wa wabunge waliotoka nje ya bunge kulalamikia matokeo hayo ni wa chama cha Kiislamu cha Muungano kwa ajili ya Algeria ya Kijani ambao licha ya watabiri na wataalamu wengi wa mambo kutabiri kwamba wangepata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo, lakini walifanikiwa kupata viti 60 tu kati ya viti vyote 462 vya bunge hilo. Kwa miaka mingi wagombea wa Kiislamu wamekuwa wakizuiwa kujishughulisha na masuala ya kisiasa nchini humo lakini watawala wa nchi hiyo walilazimika kuwaruhusu washiriki kwenye harakati za kisiasa nchini baada ya kushuhudia mwanko wa Kiislamu uliowang'oa madikteta wa nchi nyingine za Kiarabu na hivyo kuhofia kwamba mwamko huo ungewakumba na wao. Pamoja na hayo lakini kungali kuna matatizo makubwa katika sheria za uchaguzi ambazo zinabana na kuwazuia wagombea wenye misimamo ya Kiislamu kushiriki vyema kwenye chaguzi za nchi hiyo. 1017422