IQNA

Hizbullah ya Lebanon yalaani mauaji ya kutisha ya al-Hawla nchini Syria

12:08 - May 28, 2012
Habari ID: 2335933
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, imetoa taarifa ikilaani vikali mauaji yaliyotekelezwa hivi karibuni na magenge ya magaidi wa Syria huko katika eneo la al-Hawla karibu na mkoa wa Homs.
Magenge hayo yametekeleza kitendo hicho cha kinyama na kuua watu wengi wasio na hatia wakiwemo watoto wadogo. Taarifa hiyo imesema kwamba Hizbullah imesikitishwa na kushangazwa mno na mauaji hayo ya kutisha yaliyotekelezwa na magenge ya watu wasiojali utu wa mtu. Imesema Hizbullah daima imekuwa ikibainisha wazi misimamo yake kuhusiana na masuala mbalimbali ya Syria na kusisitiza kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee muafaka ya kutatuliwa mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo. Imewataka wapinzani wa serikali ya Syria kurejea kwenye meza ya mazungumzo na viongozi wa serikali na kutowategemea wageni katika utatuzi wa matatizo ya nchi hiyo au katika marekebisho muhimu ya kisiasa nchini kwa. Katika kudumisha vitendo vya vya ugaidi dhidi ya raia wasio na hatia wa Syria magenge ya kigaidi ya nchi hiyo hivi karibuni yalitekeleza mauaji ya kutisha katika eneo la al-Hawla ambapo watu wasio na hatia wapatao 90 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa kinyama. Magenge hayo yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi na kieneo na hasa Saudi Arabia, Qatar na Uturuki yanafanya njama za kuing'oa madarakani serikali halali ya Damascus kupitia njia za kigaidi, mauaji na uharibifu wa mali ya umma nchini humo. 1018377
captcha