IQNA

Mrengo wa Sadr nchini Iraq wawasilisha mashtaka dhidi ya Terry Jones

17:13 - May 29, 2012
Habari ID: 2337181
Mrengo wa Muqtada Sadr nchini Iraq umewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya Kasisi Terry Jones wa jimbo la Florida nchini Marekani kwa kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Muqtada Sadr mwenyewe amesema anaunga mkono kikamilifu juhudi za kutaka kufikishwa mahakamani kasisi huyo kutokana na hatua yake ya kuchoma moto kitabu hicho cha mbinguni. Mwaka uliopita na kufuatia kitendo cha kasisi huyo mwovu cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu, Muqtada Sadr aliutaja mwaka huo kuwa ni Mwaka wa Qur'ani nchini Iraq na kufanya juhudi kubwa za kuimarisha shughuli za Qur'ani ndani na nje ya nchi hiyo. Terry Jones amechoma moto mara mbili kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika jimbo la Florida ikiwa ni katika hatua yake ya kueneza chuki na uadui dhidi ya Uislamu. Pia ameandika kitabu cha kichochezi kinachoitwa 'Uislamu Unatokana na Shetani' ili kufikia lengo lake hilo la kishetani. 1019053
captcha