Sheikh Ibrahim Yaqub Zakzaki, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amelaani mauaji yaliyotekelezwa hivi karibuni dhidi ya mwanazuoni mmoja wa Kishia katika Husseiniya ya Baqiyatullah (af) mjini Zaria.
Maqaidi walivamia husseiniya hiyo hivi karibuni na kumuua shahidi Sheikh Ibrahim Sidi akiwa na wenzake wawili pamoja na kuwajeruhi wengine kadhaa wanachama wa Harakati ya Kiislamu. Amesema magaidi hao walitaka kumuua Sheikh Mustafa Sidi mwakilishi wa harakati hiyo katika mji wa Potuskim lakini hawakufanikiwa kufikia lengo hilo. Sheikh Zakzaki amewataka Waislamu na wananchi wa Nigeria kuwaombea dua watu waliojeruhiwa katika tukio hilo la kigaidi ili wapate nafuu haraka. 1020797