IQNA

Wapalestina Ghaza wakumbukwa mwaka wa 45 wa 'Siku ya Naksa'

13:11 - June 05, 2012
Habari ID: 2340367
Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza leo Juni 5 wanakumbukwa mwaka wa 45 wa 'Siku ya Naksa'. Katika siku hii Wapalestina walitimuliwa kutoka ardhi zao baada ya vita vya siku sita vya mwaka 1967.
Itakumbukwa kuwa Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita muwafaka na tarehe 5 Juni 1967, vilianza vita vikubwa vya tatu kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu. Katika siku kama ya leo kikosi cha anga cha utawala ghasibu wa Israel kilifanya shambulizi la kushtukiza na kuvuka mipaka ya nchi tatu za Misri, Syria na Jordan na kufanya uharibifu mkubwa. Baada ya shambulizi hilo, vikosi vya nchi kavu vya Israel vikiwa na silaha za kisasa na uungaji mkono wa Marekani na Uingereza, vilifanikiwa kuyashinda majeshi ya Misri, Syria na Jordan katika kipindi cha siku sita tu.
1023155
captcha