IQNA

Mahakama ya Kuwait yampa kifungo cha jela mtu aliyemvunjia heshima Mtume (saw)

18:04 - June 05, 2012
Habari ID: 2340617
Mahakama moja ya nchini Kuwait ilimpa kifungo cha miaka 10 jela Hamad an-Naqi kwa kosa la kumvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
Kwa mujibu wa gazeti la Le Figaro, mahakama hiyo ilimpa an-Naqi kifungo hicho kutokana na kosa la kumvunjia heshima Mtume (saw) pamoja na masahaba zake kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter. Askari usalama wa Kuwait walimtia mbaroni raia huyo mwezi Machi uliopita kwa kosa la kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu lakini alikanusha tuhuma hizo na kusema watu wengine ndio waliofanya kosa hilo kwa kuvuruga ukurasa wake binafsi kwenye Twitter na kuweka humo maneno yasiyokuwa yake. Ahmad an-Naqi anakabiliwa na tuhuma za kumvunjia heshima Mtume (saw) na kuchochea mifarakano katika jamii ya Kuwait. Vilevile kuidharau Saudi Arabia na Bahrain na kukejeli mafundisho ya Kiislamu ni sehemu nyingine ya tuhuma ambazo zimempelekea kupewa kifungo hicho cha miaka 10. 1022988
captcha