IQNA

Alqaida yatangaza kuhusika na shambulio la kigaidi dhidi ya Mashia wa Iraq

18:56 - June 11, 2012
Habari ID: 2344547
Kundi la Mawahabi la al-Qaida nchini Iraq jana Jumapili lilitoa taarifa likitangaza kuhusika na mlipuko uliotokea hivi karibuni katika idara ya wakfu ya Mashia nchini humo, shambulio ambalo lilipelekea watu 136 kupoteza maisha na kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya lci.tf1, kundi la kigaidi la al-Qaida limetangaza kuhusika na jinai hiyo ya kutisha mjini Baghdad ambayo imetoa roho za watu na kuwajeruhiwa wengine wengi wasio na hatia. Kundi hilo lisilo na utu wala huruma limesema kuwa jinai hiyo ni kengele ya hatari kwa viongozi wa serikali ya Baghdad na wanachama wa idara iliyotajwa ya wakfu na kwamba litatekeleza jinai nyingine nyingi kama hiyo siku zijazo. Siku ya Jumatatu Juni Nne magaidi wa Kiwahabi wa kundi la al-Qaida walitega na kulipua bomu mbele ya idara ya wakfu ya Mashia mjini Baghdad ambapo watu 136 waliuawa na kujeruhiwa. 1027218
captcha