IQNA

Silaha za Hizbullah ni tukufu kutokana na kukabiliana na utawala wa Kizayuni

17:13 - June 12, 2012
Habari ID: 2345408
Najib Miqaati Waziri Mkuu wa Lebanon amesema kwamba silaha za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah ni tukufu kutokana na kupambana kwake na utawala haramu wa Israel.
Akizungumza hapo jana Jumatatu, Miqaati alisema kuwa kuna baadhi ya mirengo nchini Lebanon ambayo ina wasiwasi kuhusiana na silaha za Hizbullah lakini ameitaka kuwa na utulivu kwa kuiambia kwamba silaha hizo kamwe hazitatumika dhidi yao.
Waziri Mkuu wa Lebanon amekaribisha wito uliotolewa hivi karibuni na Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah wa kuitaka mirengo na makundi yote ya kisiasa ya Lebanon yakutane na kufanya mazungumzo ya kuimarisha umoja na mshikamano nchini.
Akiashiria ghasia za hivi karibuni nchini humo Miqaati amesema kuwa, kuna mikono ya kigeni inayojaribu kuzusha fitina na vurugu nchini humo lakini akaongeza kuwa moto wa fitina hiyo umezimwa kutokana na hatua za kimantiki zilizochukuliwa na serikali pamoja na taifa la Lebanon. 1028145
captcha