Adel El-Gogari amesema kuwa lengo la kuenezwa fikra hizo ni kudhoofisha nchi za Kiarabu na kuzuia wimbi la mwamko wa Kiislamu kuiathiri nchi hiyo, ili iweze kuwa nchi pekee yenye nguvu katika Mashariki ya Kati sambamba na utawala wa Israel, ambalo ndilo lengo linalofuatiliwa na watawala wa Marekani. Amesema fikra hizo ni hatari kwa sababu uwahabi unashirikiana kwa karibu na makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya dunia, jambo linalohatarisha usalama wa jamii nzima ya mwanadamu.
El-Gogari ameongeza kuwa hakuna sehemu yoyote ya dunia ambapo vitendo vya ugaidi unaoshirikiana na utawala haramu wa Israel au Marekani havionekani. Amesema Uwahabi hii leo unatumia televisheni nyingi za satalaiti kwa jina la dini ili kuendesha vitendo vya ugaidi, fitina na kuwakufurisha Waislamu ulimwenguni. Amesema jambo hilo linaonekana wazi nchini Syria ambako Mawahabi wanashirikiana kwa karibuni na Marekani pamoja na Wazayuni wa Israel kwa ajili ya kuvuruga amani na uthabiti wa nchi hiyo.
El-Gogari amesema Mawahabi wamekuwa wakitumia fedha nyingi kufadhili mipango ya ugaidi na ukufurishaji wa Waislamu ili kufikia lengo la kuwa na ushawishi na nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati kwa ushirikiano wa nchi za Magharibi na Wazayuni.
El-Gogari ameongeza kuwa hivi sasa fikra za uwahabi zinaonekana wazi katika nchi za Misri, Syria, Libya, Tunisia na hata Iraq ambako Mawahabi wamekuwa wakimwaga fedha nyingi kwa lengo la kuiangusha serikali ya Nuri al-Maliki.
Hivi karibuni serikali ya Saudia ilitumia dola milioni 500 kwa lengo la kutaka kuiangusha serikali ya Baghdad. 1029019