Kwa mujibu wa tovuti ya trouvetamosquee, utafiti na uchunguzi huo unaonesha kwamba watu wanaojiarifisha katika nchi hizo kuwa wapinzani wa Uyahudi ndio walewale wanauopiga vita Uislamu.
Ripoti ya utafiti huo inaoonyesha kwamba Waislamu na Mayahudi wanaopigwa vita na kubaguliwa katika nchi za Magharibi wana hisia inayofanana kuhusiana na suala hilo, jambo ambalo taratibu linaimarisha umoja na mshikamano kati yao.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo Waislamu na Mayahudi wamekuwa wakiandaa makongamano na mijumuiko ya pamoja kwa lengo la kupanga mikakati ya pamoja ya kukabiliana na chuki na ubaguzi dhidi yao. 1029006