IQNA

Mkutano wa maulamaa wa Kiislamu na Kikristo kufanyika Lebanon

18:11 - June 16, 2012
Habari ID: 2347933
Mkutano wa maulamaa wa Kiislamu na Kikristo umepangwa kufanyika Jumatatu ya tarehe 18 Juni katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Gazeti la al Intiqad linalochapishwa Lebanon limemnukuu Sheikh Malik al Shiar ambaye ni Mufti wa eneo ya Tripoli huko kaskazini mwa Lebanon akitaka kufanyika mkutano huo utakaohudhuriwa na maulamaa wa Kiislamu na Kikristo.
Mkutano huo utafanyika kwa kaulimbiu ya "Kuasisi Amani kwa Ushirikiano wa Waislamu na Wakristo" katika ukumbi wa mikutano wa Msikiti wa Muhammad Amin.
Mkutano huo utakaofanyika kwa ushirikiano wa al Azhar, utahudhuriwa na Askofu Mkuu wa Wakristo wa Kimaroni wa Lebanon Mar Bishara Petros, ujumbe wa Vatican utakaoongozwa na Kadinali Jean-Louis Pierre Tauran, ujumbe wa kanisa la Anglikana, na Askofi Mkuu wa Washington.
Ujumbe wa Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mkutano huo utaongozwa na Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiisalmu. Vilevile utahudhuriwa na ujumbe wa Darul Iftaa ya Tripoli huko Lebanon.
1031084

captcha