IQNA

Ahmadinejad: Umoja wa Misri na Iran utavunja njama za utawala wa Kizayuni

15:04 - June 17, 2012
Habari ID: 2348463
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuimarishwa umoja baina ya Iran na Misri ndio njia bora zaidi ya kuangamiza satuwa ya madola ya kibeberu na utawala haramu wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na familia za wanamapinduzi waliouawa shahidi Misri wakati wa mwamko uliopelekea kutimuliwa dikteta Hosni Mubarak.
Ahmadinejad ameongeza kuwa habari za umoja baina ya Iran na Misri zinatosha kuwatimua Wazayuni kutoka katika eneo hili.
Rais wa Iran amesema Wazayuni wameshatangaza kuwa hawatosheki na kupora ardhi za Palestina bali wanapanga kukalia kwa mabavu ardhi za mataifa mengine kwa hivyo umoja wa nchi za eneo utazima njama hizo za Wazayuni. Ahmadinejad ameongeza kuwa Iran iko tayari kutumia uzoefu wake kulisaidia taifa la Misri lipige hatua kimaendeleo.
1031670
captcha