Ukikamilika, msikiti huo unatarajiwa kuwa nembo ya kukua kwa kasi Uislamu nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mahakama hiyo imebatilisha hukumu ya Oktoba mwaka jana iliyotolewa na Mahakama Ndogo ya Marseille iliyobatilisha ujenzi wa msikiti huo kwa kisingizio kuwa ujenzi wake ungekiuka mpango wa mji.
Msikiti huo utakaogharimu Euro milioni 22 utajumuisha ukumbi mkubwa wa msikiti wenye uwezo wa kubeba watu 7,000 na mnara wenye urefu wa mita 25.
Viongozi wa Kiislamu mjini Marseille wamepongeza uamuzi huo wa mahakama na kusema ni hatua muhimu katika kutambua umuhimu wa jamii kubwa ya Waislamu katika mji huo ulio katika pwani ya Mediterranean.
Mji huo wa pili kwa ukubwa Ufaransa una takribani Waislamu laki mbili na nusu ambao aghalabu huswali katika maeneo madogo na duni.
Ufaransa ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya ambapo kuna karibu Waislamu milioni tano hadi sita na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi. Hivi sasa Uislamu ndio dini ya pili kwa idadi nchini Ufaransa.
1034217