Ali Larijani ameyasema hayo mjini Tehran katika mkutano na Maher Taher mwanachama wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina.
Larijani amesisitiza kuwa, leo zaidi ya wakati wowote ule, utawala wa Kizayuni umetengwa. Kuhusiana na kadhia ya Syria, Spika wa Bunge la Iran amesema serikali ya Syria iko katika mstari wa mbele kutetea taifa la Palestina na kuupinga utawala wa Kizayuni na hii ndio sababu inalengwa na maadui.
Kwa upande wake Maher Taher amepongeza sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuunga mkono taifa la Palestina. Afisa huyo wa Palestina amesema Waislamu wanapaswa kuungana ili kukabiliana na njama za nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na Utawala wa Kizayuni.
1036655