IQNA

Israel yakumbwa na msiba juu ya ushindi wa Mursi, Hamas yafurahi

13:31 - June 25, 2012
Habari ID: 2354028
Utawala ghasibu wa Israel umekumbwa na wasiwasi mkubwa kufuatia ushindi wa harakati ya Ikhwanul Muslimina nchini Misri.
Utawala huo ulibainisha wasiwasi huo hapo jana baada ya kutangazwa ushindi wa Muhammad Mursi na kuongeza kuwa, ushindi huo utasababisha kuharibika uhusiano uliokuwepo kati ya Israel na Misri. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, wasiwasi huo unatokana na kuwepo uwezekano wa kuvunjika kwa mkataba wa Camp David uliotiwa saini mwaka 1978 na watawala wa zamani wa nchi hizo. Nayo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa pongezi kwa wananchi wa Misri kufuatia ushindi huo na kuongeza kuwa, ushindi wa Muhammad Mursi ni tukio muhimu katika historia ya taifa la Misri na kuhitimishwa ushirikiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni. Hayo yalisema hapo jana na msemaji wa harakati hiyo Sami Abu Zuhri na kuongeza kuwa, ushindi huo umewafurahisha pia wananchi wa Wapalestina hususan wakazi wa Ukanda wa Gaza ambao wamekuwa katika mzingiro wa muda mrefu unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni.
1037395
captcha