Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni Duniani la Umoja wa Mataifa (UNESCO), limepitisha kwa wingi wa kura ombi la Palestina la kutaka eneo alikozaliwa Nabii Isa (as) (Church of Nativity) liorodheshwe kama turathi ya Dunia.
Wanachama 13 wa UNESCO wamepitisha ombi hilo dhidi ya kura 6 zilizolipinga. Utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na Marekani zilipinga ombi hilo na zimeilaumu UNESCO kwa kukubali ombi la Wapalestina. Mjumbe wa Palestina katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa ameitaja hatua hiyo kama hatua ya kwanza ya kuzilinda ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Palestina ilikuwa imeiomba UNESCO kuhifadhi eneo hilo katika mji wa Baitul-laham baada ya kukithiri ujuba wa Israel unaolikalia eneo hilo kwa mabavu. Aidha njia ya wanaoenda kuzuru eneo hilo pia imetangazwa kuwa ni turathi
1040892