Mkuu wa Taasisi ya Mazungumzo Kati ya Tamaduni Tofauti ya Russia katika mazungumzo yake na Ayatullah Ali Taskhiri, Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhebu ya Kiislamu ya Iran, amesifu msimamo wa pamoja wa nchi mbili hizi kuhusiana na mgogoro wa Russia.
Ayatullah Taskhiri ambaye amekuwa nchini Russia kwa lengo la kushiriki katika kongamano la nane la mazungumzo baina ya tamaduni amekutanana kubadilishana mawazo na Vladimir Yakunin, Mkuu wa Taasisi ya Mazungumzo kati ya Tamaduni Tofauti ya Russia kuhusiana na masuala mbalimbali ya kieneo na kimataifa.
Yakunin pia amesifi uhusiano mzuri wa kiutamaduni na kisiasa uliopo baina ya pande mbili na kutangaza kuridhishwa kwake na msimamo wa pamoja wa hivi karibuni wa nchi hizo kuhusiana na suala la Syria.
Amesema Iran daima imekuwa ikisisitiza juu ya kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kutatua matatizo na changamoto tofauti zinazoukabili ulimwengu wa leo.
Kwa upande wake Ayatullah Ali Taskhiri amesisitiza juu ya umuhimu wa kuchukuliwa msimamo mmoja katika kukabiliana na maadui wanaotaka kuvuruga usalama na amani ya eneo muhimu la Mashariki ya Kati. 1040620