IQNA

Msikiti Mkubwa zaidi Asia ya Kati wafunguliwa Kazakhstan

15:23 - July 09, 2012
Habari ID: 2364426
Msikiti mkubwa zaidi Asia ya Kati umefunguliwa nchini Kazakhstan miezi sita baada ya jengo hilo kuteketea wakati ujenzi wake ulipokuwa ukiendelea.
Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan alihudhuria sherehe za kufunguliwa msikiti huo katika mji mkuu wa nchi hiyo Astana. Ufunguzi huo umesadifiana na kumbukumbu ya mwaka wa 14 wa kuasisiwa mji huo.
Msikiti huo una ukubwa wa mita mraba 17,500 na kuba lenye ukubawa wa mita 51 kati kati na makuba mengine manane madogo madogo.
Karibu asilimia 70 ya wakaazi milioni 16 wa nchi hiyo iliyokuwa katika shirikisho la zamani la Sovieti ni Waislamu. Aghalabu ya Wakazakh ni wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi.
Jengo la msikiti huo liliteketea Januari mwaka huu baada ya mashine ya kuchomelea vyuma kushika moto.
1048530
captcha