IQNA

Majlisi ya Mashia wa India (AISPLB) yataka utengenezaji wa filamu inayozungumzia Karbala usimamishwe

13:57 - July 19, 2012
Habari ID: 2372533
Majlisi ya Mashia wa India AISPLB imeitaka serikali ya nchi hiyo iingilie kati na kusimamisha utengenezaji wa filamu inayozungumzia matukio ya Karbala inayoendelea kutengenezwa katika sekta ya filamu ya nchi hiyo Bollywood.
Majlisi hiyo imemwandikia barua Waziri Mkuu na Waziri wa Habari wa India ikiwataka waingilie kati na kusimamisha mara moja utengenezaji wa filamu hiyo kwa sababu inadhuru hisia za Waislamu. Akitoa taarifa kuhusiana na suala hilo, Maulana Reza Muhammad At'har mkuu wa majlisi hiyo amesema kutokana na kuwa sifa za Imam Hussein (as) ambaye anaenziwa na kutukuzwa na mamilioni ya Waislamu duniani zitazungumziwa katika filamu hiyo na kupelekea kudhuriwa hisia zao, majlisi hiyo inaitaka serikali iingilie kati mara moja na kusimamisha utengenezaji wake. Amesema kwa mtazamo wa sheria za Kiislamu, utengenezaji wa filamu kama hiyo inayowahusu watu mashuhuri na watukufu wa kidini ni jambo lisiloruhusiwa. 1056878
captcha