Hussein Naqavi-Husseini msemaji wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Iran amesema Iran itaongoza juhudi za kimataifa za kuwasaidia Waislamu waliowachache wanaokandamizwa Myanmar.
Wakati huo huo Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu imelaani mauaji ya Waislamu Myanmar na kuitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua za haraka kusitisha mauaji hayo ya umati. Taarifa ya jumuiya hiyo yenye makao yake Tehran mbali na kulaani mauaji ya maelfu ya Waislamu na kuhujumiwa watoto na wanawake imetoa wito kwa watu wa dini zote nchini humo kuishi kwa amani.
Tokea mwezi Juni mwaka huu wa 2012, maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar. Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 katika nchi hiyo ya mashariki mwa Asia.
1056815