Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus Erato Kozakou-Marcoullis ambaye nchi yake inashikilia uenyekiti wa mzunguko wa EU amesema hakuna muafaka miongoni mwa nchi zote za Ulaya kuhusu kuiweka Hezbollah katika orodha ya mashirika ya kigaidi.
Kozakou-Marcoullis amesema Hizbullah ni shirika lenye mrengo wa kijeshi na ambalo pia linashiriki kikamilifu katika siasa za Lebanon.
Utawala haramu wa Israel umekuwa ukieneza tuhuma zisizo na kimsingi dhidi ya Hizbullah. Propaganda hizo za Israel zinatokana na kuwa utawala huo umepata pigo mara kadhaa kutoka kwa wapiganaji shupavu wa Hizbullah.
Pigo kubwa zaidi ulilipata utawala wa Kizayuni wa Israel kutoka Hizbullah ni katika vita vya siku 33 vya Israel dhidi ya Lebanon mwaka 2006.
1062300