IQNA

Polisi ya Punjab kuanza shughuli zake za kila siku kwa kusoma Qur'ani

12:11 - July 30, 2012
Habari ID: 2380776
Kwa mujibu wa maagizo mapya yaliyotolewa na polisi ya jimbo la Punjab nchini India, vituo vyote vya polisi katika jimbo hilo vitakuwa vikianza shughuli zao za kila siku za kiidara kwa kusoma Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Nation, maagizo hayo yametolewa na Muhammad Habib ar-Rahman Mhasibu Mkuu wa Idara ya Polisi katika mkoa huo.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wa idara ya polisi katika jimbo la Punjab, maagizo hayo yametolewa kwa idara na vituo vyote vya polisi vikiwemo vya masomo katika mkoa huo. 1064963
captcha