Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kufuatia kutekwa nyara wafanyaziara 48 wa Kiirani nchini Syria. Msemaji wa Ban Ki-moon amewaambia waandishi wa habari kuwa, Umoja wa Mataifa unafuatilia suala la kutekwa nyara raia wa Iran nchini Syria na utatoa kauli yake karibuni hivi kuhusu jambo hilo.
Wakati huo huo, Bw. Kazem Jalali, mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema kuwa, Uturuki inapaswa kubeba jukumu la kutekwa nyara raia 48 wa Iran nchini Syria. Amesema, jukumu la kulinda usalama wa raia hao wa Iran liko mabegani mwa Uturuki na nchi zote zinazoyasaidia makundi ya kigaidi nchini Syria.
Itakumbukwa kuwa, Jumamosi iliyopita, makundi ya watu wenye silaha yaliliteka nyara basi lililokuwa na raia 48 wa Iran waliokuwa katika barabara ya Uwanja wa Ndege mjini Damascus.
1072272