Kwa mujibu wa tovuti ya Bernama, Bwana Mahathir Muhammad amesema kwamba ana yakini kuwa iwapo Waislamu wote katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu wataungana na kuwatetea kwa pamoja Waislamu wa Myanmar, bila shaka Umoja wa Mataifa nao utalazimika kuchukua hatua za lazima kuhusiana na suala hilo.
Mahathir Muhammad pia ameitaka serikali ya Myanmar kuchukua hatua za kuwalinda Waislamu hao Rohingya.
Hivi karibuni maelfu ya Waislamu wa Malaysia na wakimbizi Waislamu wa Rohingya walifanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa nchi hiyo mjini Kuala Lumpur kwa ajili ya kulaani mauaji ya kizazi yanayofanywa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya Waislamu na kutaka yasimamishwe mara moja.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba ikiwa mwanachama hai na mwenye nguvu wa jumuiya ya ASEAN, Malaysia ina uwezo wa kuwashawishi wanachama wengine wa jumuiya hiyo wachukue hatua za lazima kwa lengo la kusimamisha mauaji hayo dhidi ya Waislamu wasio na hatia wa Myanmar. 1075670