Mbunge huyo mwenye misimamo mikali ya Kiyahudi ambaye aliwahi kutoa pendekezo la kubadilishwa eneo la Msikiti wa al Aqsa, amewasilisha muswada wa kugawanywa Msikiti wa al Aqsa katika bunge la Israel.
Muswada huo unasisitiza juu ya kutengwa wakati maalumu kwa ajili ya Mayahudi kuzuru Msikiti wa al Aqsa, kutekeleza ibada katika eneo hilo takatifu na kuwazuia Waislamu kuingia katika msikiti huo isipokuwa katika vipindi maalumu.
Sheikh Kamal al Khatib ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina inayokaliwa kwa amabavu ametahadharisha kuhusu muswada huo na kusisitiza kuwa Msikiti wa al Aqsa ni haki na mali ya Waislamu. 1075869