IQNA

ISESCO yalaani uamuzi wa utawala wa Israel wa kubadilisha eneo la msikiti wa al Aqsa

14:00 - August 12, 2012
Habari ID: 2391006
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni ya Jumuiya ya ushifrikiano wa Kiislamu ISESCo limetoa taarifa likilaani matamshi yaliyotolewa na mbunge mmoja wa Israel aliyetaka kubadilishwa eneo la msikiti wa al Aqsa.
ISESCO imezitaka nchi wanachana wa OIC na jamii ya kimataifa kuchukua msimamo imara dhidi ya utekelezaji wa mpango huo muovu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wakati huo huo mbunge mmoja wa Israel amewasilisha muswada wa kugawanywa Msikiti mtakatifu wa al Aqsa kati ya Waislamu na Wayahudi.
Mbunge huyo mwenye misimamo mikali ya Kiyahudi ambaye aliwahi kutoa pendekezo la kubadilishwa eneo la Msikiti wa al Aqsa, amewasilisha muswada wa kugawanywa Msikiti wa al Aqsa katika bunge la Israel.
Muswada huo unasisitiza juu ya kutengwa wakati maalumu kwa ajili ya Mayahudi kuzuru Msikiti wa al Aqsa, kutekeleza ibada katika eneo hilo takatifu na kuwazuia Waislamu kuingia katika msikiti huo isipokuwa katika vipindi maalumu.
Sheikh Kamal al Khatib ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina inayokaliwa kwa amabavu ametahadharisha kuhusu muswada huo na kusisitiza kuwa Msikiti wa al Aqsa ni haki na mali ya Waislamu. 1075084

captcha