Kongamano hilo ambalo linahudhuriwa na Said Jalili, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa la Iran miongoni mwa shakhsia wengine mashuhuri, limeandaliwa na Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu kwa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds Tukufu.
Lengo la kuandaliwa kongamano hilo limetajwa kuwa ni kunufaika na mitazamo na ujuzi wa wasomi kwa lengo la kuandaa ramani ya njia ya kuikomboa Quds Tukufu. Ramani hiyo imepangwa kutayarishwa katika fremu ya matukio ya hivi karibuni kaskazini mwa Afrika na mashariki ya Kati na kwa kutegemea miongozo muhimu ya hayati Imam Khomeini (MA) na Ayatullahil Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Kongamano hilo linahudhuriwa pia na maafisa wa ngazi za juu za kijeshi na kidiplomasia kutoka nchi za Kiislamu na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Palestina. 1077357