Kwa mujibu wa tovuti ya lorientlejour, Kamati ya Masuala ya Kisheria ya Taasisi ya Allama Muhammad Hussein Fadhlullah jana ilitoa taarifa ikisema kuwa kwa kuzingatia kuwa siku ya Jumapili itakuwa siku ya Idi, siku ya mwisho ya Mashia kufunga itakuwa siku ya Jumamosi tarehe 18 Agosti.
Kwa upande wa pili, Darul Fatawa ya Lebanon ambayo ndiyo taasisi kuu inayoshughulika masuala ya sheria za Kiislamu nchini humo kwa Masuni, hadi sasa haijatangaza siku rasmi ya kusherehekewa Idul Fitr na kwa hivyo wafuasi wa madhehebu hiyo wangali wanasubiri kutangazwa kwa siku hiyo. 1078305