Kwa mujibu wa ripoti hiyo Sharaf as-Sufyani, mwanachama wa Muungano wa Kiarabu wa Taaluma ya Nyota ambaye pia ni Naubu Mkuu wa Jumuiya ya Nyota ya Saudi Arabia amesema kuwa hilali ya mwezi wa Shawal haitaweza kuonekana Ijumaa magharibi kabla ya kutua jua. Amesema kwa kuzingatia suala hilo siku ya Jumamosi ndiyo itakuwa siku ya mwisho ya mfungo wa mwezi Ramadhini na kuwa idi itasherehekewa nchini humo siku ya Jumapili Agosti 19.
Wakati huohuo kamati ya kutazama hilali ya mwezi wa Shawal nchini Imarati imetangaza kuwa nchi nyingi za Kiislamu, na hasa zile zilizoanza funga Ijumaa ya tarehe 20 Julai zitasherehekea Idul Fitr siku ya Jumapili.
Taarifa ya muungano huo imesema kwamba kabla ya kuanza funga ya Ramadhini nchi za Kiislamu ziligawanyika katika makundi mawili ambapo baadhi ya nchi zilianza kufunga siku ya Ijumaa Juni 20 na nyingine kama vile, Indonesia, Mlaysia, Brunei, Pakistan, India, Iran, Afrika Kusini, Kenya, Tanzania, Uganda, Iraq, Oman, Syria, Morocco na Mauritania zikifunga siku iliyofuata ya Jumamosi tarehe 21.1077775