Kwa mujibu wa tovuti ya lematin, meya huyo amekubali ombi la Waislamu la kutengwa idi zao kuwa siku za mapumziko kufuatia maombi ya mara kwa mara ya viongozi wa Kiislamu kwa viongozi wa Ujeruimani kuhusiana na suala hilo.
Hamburg limekuwa jimbo la kwanza nchini humo kutoa fursa hiyo ya mapumziko kwa Waislamu. Baada ya kukutana hapo jana Jumanne na viongozi wa vituo vya Kiislamu vya kaskazini mwa Ujerumani, wanachama wa bodi ya uongozi ya Baraza la Mji wa Hamburg walisema kuwa kuanzia sasa idi za Kiislamu zitakuwa zikiwekwa kwenye kalenda za jimbo hilo kama siku rasmi za mapumziko ambapo wanafunzi na wafanyakazi wa Kiislamu wataweza kujumuika na familia zao kwa lengo la kusherehekea idi hizo.
Huku akibainisha kuwa fursa kama hiyo tayari imetolewa kwa Wakristo na Mayahudi, Meya Olaf Scholz amesisitiza kwamba kuna maelfu ya Waislamu wanaoishi mjini Hamburg ambao nao kama walivyo wafuasi wa dini nyinginezo, wana haki ya kunufaika na sikukuu zao za kidini.
Fursa hiyo imetolewa kwa Waislamu katika hali ambayo makundi yenye misimamo mikali ya kulia yanayopinga Uislamu mapema yalitisha kuwa mwishoni mwa wiki hii yatakusanyika mbele ya msikiti mkuu wa Berlin kwa lengo la kulalamikia kile yanachodai kuwa ni kufanywa Ujerumani kuwa nchi ya Kiislamu. 1079447