IQNA

Makundi ya kujitolea Malaysia kuelekea Myanmar kwa ajili ya kusaidia Waislamu

18:21 - August 21, 2012
Habari ID: 2396680
Jumuiya ya Putra ya Malaysia wiki ijayo itaelekea nchini Myanmar ikipeleka misaada ya kibinadamu kwa Waislamu wanaoendelea kukandamizwa nchini humo.
Tovuti ya The Star imeripoti kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo Datuk Aziz Abdul Rahim amesema karibu watu 45 wengi wao wakiwa madaktari, wametangaza kuwa wako tayari kuelekea Myanmar tarehe 25 Agosti. Kundi jingine litaelekea huko tarehe 2 Septemba kwa ajili ya kuendelea kutoa misaada ya Waislamu wa Myanmar wanaouawa katika hujuma inayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wakisaidiwa na jeshi la nchi hiyo.
Aziz Abdul Rahim pia amewataka waandishi na vyombo vya habari kusaidiana na ujumbe huo unaoelekea Myanmar.
Jumuiya ya Putra imesema lengo la safari hiyo ni kufikisha misaada ya chakula na dawa kwa Waislamu wanaodhulumiwa. Jumuiya hiyo pia imesema baada ya kurejea kutoka Myanmar wanachama wake wataelekea nchini Iran kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na mtetemeko wa ardhi katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki huko magharibi mwa Jamhuri ya Kiislamu. 1081685

captcha