IQNA

Mashindano ya hifdhi ya Qur’ani kufanyika Britani na Ireland ya Kusini

0:13 - August 27, 2012
Habari ID: 2399455
Mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu yamepangwa kufanyika kote Britani na Ireland ya Kusini mwezi baadaye mwaka huu.
Mashindano hayo yatasimamiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Right Star ya Britani katika miji minne ya Middelsbro, London, Dublin na Manchester.
Mashindano hayo yataanzia katika mji wa Middelsbro na kumalizikia katika mji wa Manchester. Washiriki watachuana katika makundi matatu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 10, chini ya miaka 16 na miaka 16 na kuendelea.
Mwishoni mwa mashindano hayo washindi wataenziwa na kutunukiwa zawadi.
Mashindano hayo yatafanyika kwa lengo la kuwakusanya makarii na wanachama wa misikiti na shule za Kiislamu kote Britani na Ireland, kuanzisha anga ya ushindani na kuwahamasisha wanafunzi kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu. 1085186
captcha