Gomez, anayewania nafasi ya uwakilishi katika jimbo la 31 la Texas, alichapisha video iliyosambaa kwa kasi ikimuonesha akiteketeza moto nakala ya Qur'ani Tukufu.
Katika video hiyo, aliandika maneno ya kuchochea: “Nitamaliza Uislamu Texas, Mungu nisaidie,” na kudai kuwa “Marekani ni taifa la Kikristo” huku akiwataka Waislamu waondoke kwenda “moja ya mataifa 57 ya Kiislamu.”
Kauli na video hiyo zimezua ghadhabu kubwa kutoka kwa mashirika ya kutetea Waislamu, viongozi wa kisiasa, na taasisi za kiraia. Tangu wakati huo, Gomez amepigwa marufuku kutumia mitandao yote mikuu ya kijamii isipokuwa X. Hata hivyo, hakuna uchunguzi wa uhalifu wa chuki ulioanzishwa kuhusu tukio hilo.
Katika tamko lake, Taghizadeh alinukuu Qur'an akisema: "Je, hawajui kuwa anayempinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi kwa hakika moto wa Jahannamu ni wa kwake, atadumu humo milele? Hiyo ndiyo fedheha (hizaya) kubwa." (Qur'an 9:63)
Alieleza kuwa kitendo hicho ni sehemu ya historia ndefu ya chuki na uadui dhidi ya Uislamu, kuanzia mashambulizi ya kijeshi hadi upotoshaji wa vyombo vya habari , ambavyo vyote vimeshindwa kuuzima mwanga wa imani.
Akinukuu aya nyingine, alisema: "Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu ataikamilisha nuru Yake, ijapokuwa makafiri watachukia." (Qur'an 61:8)
Aidha, alieleza kuwa chuki kama hiyo si jambo jipya, akirejea aya ya Qur'an: "Wayahudi hawataridhika nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate dini yao." (Qur'an 2:120) Taghizadeh alihusisha hili na kile alichokiita “tabia ya kuendelea ya madola ya kibabe, hasa Marekani na utawala wa Kizayuni.”
Msomi huyo wa Kiislamu kutoka Iran amesema kuwa tukio hilo linaonesha haja ya dharura ya mshikamano miongoni mwa Waislamu, akitaja Qur'an: "Shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msifarakane." (Qur'an 3:103)
Akizungumza kuelekea Wiki ya Umoja wa Kiislamu, aliwahimiza Waislamu duniani kote kuungana kwa misingi ya Qur'an na mafundisho ya Mtume (SAW) ili kukabiliana na njama dhidi ya Uislamu.
Alisisitiza kuwa “umoja huu mtukufu” ni ngao thabiti dhidi ya mashambulizi ya kitamaduni, kisiasa, na kidini.
3494407