IQNA

Waislamu wa Pakistan wamwombea msamaha Mkristo aliyevunjia heshima Qur’ani

14:54 - August 29, 2012
Habari ID: 2401387
Maulamaa na wananchi Waislamu wa Pakistan wametoa wito wa kusamehewa na kuachiwa huru msichana kijana wa Kirkisto aliyevunjia heshima Qur’ani Tukufu ambaye inasemekana anasumbuliwa na matatizo ya kiakili.
Tovuti ya OnIslam imeripoti kuwa, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Pakistan Tahir Ashrafi amesema kuwa faili hilo ni mtihani kwa Waislamu wa Pakistan, jamii za waliowachache na serikali ya nchi hiyo. Amesema Waislamu hawataki kuona dhulma ikitendeka dhidi ya mtu yeyote na watafanya jitihada kuhakikisha kwamba faili hilo linafungwa.
Mshichana huyo Mkristo wiki iliyopita alikabidhiwa kwa polisi ya Islamabad baada ya kuchoma moto kurasa kadhaa za kitabu kitakatifu cha Qur’ani.
Kwa mujibu wa katiba ya Pakistan, hukumu ya mtu anayevunjia heshima matukufu ya Kiislamu ni kifo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Baraza Kuu la Maulamaa wa Kiislamu wa Pakistan kumtetea mtu asiyekuwa Mwislamu na hatua hiyo imepongezwa na viongozi wa dini nyinginezo. 1087324
captcha