IQNA

Malaysia, mwenyeji wa idadi kubwa zaidi ya watalii Waislamu

14:55 - August 29, 2012
Habari ID: 2401389
Uchunguzi mpya umebaini kuwa Malaysia kila mwaka hutembelewa na idadi kubwa zaidi ya watalii Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia.
Tovuti ya Muslim Village imeripoti kuwa matokeo ya uchunguzi huo ambao umefanyika kwa mujibu wa safari za Waislamu, yanaonesha kuwa nchi mbili za Uturuki na Imarati zinafuatia kwa kuwa wenyeji wa watalii wengi wa Kiislamu.
Baada ya nchi hizo tatu zinafuatia nchi za Singapore, Russia, China, Ufaransa, Thailand na Italia.
Uchunguzi huo umebaini kuwa asilimia 67 ya Waislamu wanachagua nchi za kutembelea kwa kutilia maanani suala la kupata vyakula halali.
Uchunguzi huo pia unaonesha kuwa sekta ya utalii ya Kiislamu hupata faida ya dola bilioni 126.1 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 12.3 ya pato la utalii kote duniani. 1087323


captcha