Gazeti la al Riyadh linalochapishwa nchini Saudi Arabia limemnukuu Mwenyekiti wa Baraza la Idara la Jumuiya hiyo Bwana Ahmad Muhammad Ali akisema kuwa mpango wa kusambaza nakala za Qur’ani zenye hati za braille unatekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi na vituo kadhaa vinavyotoa huduma kwa walemavu wa macho.
Ahmad Muhammad Ali ameongeza kwamba lengo la kutekeleza mpango huo ni kuwawezeshawalemavu wa macho kusoma Qur’ani kwa hati za braille.
Ameongeza kuwa imepangwa kuwa vituo vya Qur’ani vya ulimwengu wa Kiislamu vitashirikiana kuchapicha vitabu vya tafsiri ya Qur’ani na vya sira ya Mtume Muhammad (saw) kwa hati za braille katika kiwanda cha kuchapisha Qur’ani cha Mfalme Fahad nchini Saudi Arabia. 1090377