IQNA

Mafunzo ya Ijue Qur'ani Tukufu kuanza Afrika Kusini

18:22 - September 04, 2012
Habari ID: 2405166
Mafunzo ya muda ya "Ijue Qur'ani Tukufu; Tajiriba ya Muujiza" yataanza tarehe 11 Septemba katika Msikiti wa Cape Town nchini Afrika Kusini.
Tovuti ya CTME imeripoti kuwa mafunzo hayo yataendelea kwa kipindi cha wiki 10 katika msikiti huo wa Cape Town.
Mafunzo ya "Ijue Qur'ani Tukufu; Tajiriba ya Muujiza" yatajumuisha kiraa, tafsiri ya sura 15 fupi za Qur'ani Tukufu, mafunzo ya juzuu tatu za kwanza za Qur'ani, vikao vya maswali na majibu na maonyesho ya picha za mafunzo ya Qur'ani Tukufu.
Vilevile jana msikiti wa Darul Naeem wa Cape Town ulikuwa mwenyeji wa warsha ya Njia ya Kuelekea kwenye Qur'ani.
Warsha hiyo ya mafunzo ambayo itaendelewa kwa kipindi cha wiki tatu ni makhsusi kwa wanawake na inachunguza njia za kufaidika na Qur'ani Tukufu. 1090667

captcha