Tovuti ya Russia Today imeripoti kuwa, Kasisi Terry Jones ameanzisha harakati hiyo ya kijeuri kwa kudai kuwa mafundisho ya Nabii Muhammad yalikuwa na taathira katika mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 dhidi ya majengo mapacha mjini New York na kwa msingi huo amesema atamhukumu Mtume Muhammad (saw) tarehe 11 Septemba sambamba na kumbukumbuku za tukio hilo!
Mhubiri Mkristo wa mwenye asili ya Misri Usama Daqduq pia atafuatana na Kasisi Jones na filamu ya tukio hilo la kifidhuli itarushwa hewani na televisheni moja ya kieneo huko Marekani.
Kasisi Terry Jones wa kanisa moja la Marekani aliwahi kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika jitihada zake za kuupiga vita Uislamu.
Kundi moja vijana wa Kiislamu limelaani hatua za kasisi huyo na kutangaza kuwa misimamo dhaifu ya Waislamu ya kutokabiliana vilivyo na kasisi huyo wakati alipochoma moto nakala za Qur'ani imemshajiisha kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw). 1092181