IQNA

Maonyesho ya nakala ndefu zaidi iliyoandikwa kwa haki za mkono ya Qur'ani

22:19 - September 05, 2012
Habari ID: 2406063
Nakala ndefe zaidi duniani ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono juu kitambaa chenye urefu wa mita 208 inaonyeshwa katika mji wa Istanbul, Uturuki.
Nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu inaonyeshwa katika maonyesho ya kwanza ya kazi za kisanii na kiutamaduni za Kiislamu za China mjini Istanbul ambayo yataendelea hadi Ijumaa ijayo.
Nakala hiyo ndefu zaidi ya Qur'ani imeandikwa kwenye kitambaa chenye upana wa mita 1 na sentimita 15 na kina uzito wa kilo 86.
Nakala hiyo ya Qur'ani imeandikwa na wanakaligrafia wa kaumu za Uighur na Hui za China na hii ni mara ya kwanza kutolewa nje ya nchi hiyo kwa ajili ya maonyesho.
Sehemu moja ya maonyesho ya Istanbul, Uturuki inaonyesha kazi za kisanii za Waislamu wa China na athari za kihistoria na kiutamaduni zenye umri wa miaka 300. 1092337




captcha