IQNA

Mashindano ya 13 ya kimataifa ya Qur'ani kufanyika Russia

12:08 - September 08, 2012
Habari ID: 2407118
Mashindano ya 13 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 14 Oktoba katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
Mashindano hayo ambayo mwaka huu yatahusu hifdhi ta Qur'ani yatasimamiwa na Rais wa Baraza la Mamufti la Russia Ravi Ainuddin kwa msaada wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.
Mashindano hayo yatafanyika katika awamu mbili na mahafidhi bora watakaofaulu vizuri katika awamu ya awali watachuana katika awamu ya pili na ya mwisho.
Mahafidhi 30 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki, Ufaransa, Qazakhstan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Marekani, Indonesia, Tunisia, Afrika Kusini, China na Morocco watashiriki katika mashindano hayo.
Watayarishaji wa mashindano ya 13 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Russia wametayarisha ratiba mbalimbali zitakazofanyika katika mashindano hayo. 1093478

captcha