IQNA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran apinga madai ya William Hague

23:21 - September 09, 2012
Habari ID: 2408390
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran amesema kuwa madai yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu suala la kuzidishwa vikwazo dhidi ya Tehran yanaakisi jinsi serikali ya London isivyowajibika.
Ramin Mehmanparast amejibu madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague kuhusu miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini akisema kuwa shughuli hizo zinafanyika chini ya usimamizi kamili wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Amepinga vikali wito wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza wa kuzidishwa vikwazo dhidi ya Tehran na akasema unaakisi kutowajibika nchi hiyo katika masuala ya kimataifa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria taarifa iliyotolewa na mkutano wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) mjini Tehran na uungaji mkono wa jumuiya hiyo kwa miradi ya nyuklia ya Iran na kusema matamshi yaliyotolewa na afisa huyo wa Uingereza yanakiuka sheria za wakala wa IAEA na yametolewa kutaka kutaka kufifiza mafanikio ya mkutano wa jumuiya ya NAM mjini Tehran.
Mehmanparast amesisitiza kuwa siasa za mashinikizo sambamba na mazungumzo za nchi za Magharibi dhidi ya Iran zimefeli na ameziusia nchi hizo kuachana na fikra zilizopitwa na wakati. 1094669
captcha