IQNA

OIC yalaani mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya matukufu ya Wakristo

23:20 - September 09, 2012
Habari ID: 2408393
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani kitendo cha kuvunjiwa heshima kanisa la Wakristo katika mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) kilichofanywa na walowezi wa Kiyahudi.
Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani hujuma ya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya kanisa hilo na kitendo chao kuandika maneno yanayomvunjia heshima Nabii Issa Masih (as) katika kuta zake. Amesema kitendo hicho ni mfano wa ugaidi mpya wa walowezi wa Kiyahudi ambao wamezidisha mashambulizi dhidi ya matukufu ya Kiislamu na Kikristo.
Katibu Mkuu wa OIC amesema walowezi hao wa Kizayuni hawaheshimu matukufu na kwamba uhalifu wao unafanyika kwa uungaji mkono wa jeshi la Israel.
Katika sehemu nyingine ya taarifa yake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio unaopaswa kulaumiwa kwa vitendo hivyo vya kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Ekmeleddin Ihsanoglu ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kusimamisha mashambulizi hayo na kuzuia ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Israel.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa kundi moja la Wayahudi wenye misimamo mikali siku chache zilizopita lilivamia kanisa moja huko Quds Tukufu (Jerusalem) na kuchoma moto sehemu ya eneo hilo la ibada. 1094381
captcha