IQNA

Waislamu wa madhehebu ya Suni walaani mauaji ya Shia Pakistan

23:21 - September 09, 2012
Habari ID: 2408395
Waislamu wa madhehebu ya Suni nchini Pakistan wamefanya maandamano makubwa wakilaani mauaji yanayofanywa na makundi yenye misimamo mikali ya Kiwahaabi dhidi ya Waislamu wenzao wa madhehebu ya Shia.
Maandamano hayo yamefanyika kuonyesha mshikamano na umoja wa Waislamu hao na ndugu zao wa madhehebu ya Shia.
Katika maandamano hayo ya Waislamu wa madhehebu ya Suni maulamaa wa dini wa Pakistan wamewataka maafisa wa serikali kuhakikisha uadilifu unatendeka na kusema Waislamu wa Shia na Suni wa Pakistan wanaungana katika kulinda nchi yao na wanaelewa vyema njama zinazofanywa na maadui.
Wamesisitiza kuwa njama hizo zinazopangwa na mabeberu na nchi zinazopinga Uislamu dhidi ya wafuasi wa dini hiyo hazitafaulu. 1093464
captcha