IQNA

Maandamano yafanyika New York kupinga harakati dhidi ya Uislamu

23:21 - September 09, 2012
Habari ID: 2408397
Maandamano makubwa yamefanyika mjini New York, Marekani kupinga harakati zinazofanyika nchini humo dhidi ya Uislamu.
Viongozi wa dini mbalimbali wameshiriki pia katika maandamano hayo ya kupinga harakati zinazofanyika dhidi ya dini ya Kiislamu nchini Marekani.
Waandamanaji ambao walibeba mabango yanayopinga propaganda zinazochafua sura ya Uislamu na kuwatisha watu na dini hiyo, wametoa wito wa kukomeshwa harakati hizo.
Waandamanaji hao pia wametoa wito wa kuheshimiwa dini mbalimbali na kukomeshwa uvumi na harakati zinazowatishia watu na dini za mbinguni.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa maandamano hayo yameitishwa kutokana na nara na ujumbe unaopiga vita Uislamu uliotundikwa katika treni na chini ya ardhi (metro) katika jimbo la New York. 1094889

captcha