IQNA

Maandamano ya kupinga marufuku ya hijabu yafanyika Uturuki

8:03 - September 10, 2012
Habari ID: 2408462
Wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa katika mji wa Istanbul wakipinga marufuku ya vazi la hijabu katika shule na vyuo vikuu nchini humo.
Taasisi 12 zisizo za kiserikali za Uturuki zimetaka vazi la stara la hijabu lipewe uhuru kamili nchini humo ikiwa ni katika juhudi za taasisi hizo za kukosoa kuendelea kuzuiliwa vazi la hijabu katika shule na idara za serikali nchini humo.
Taasisi hizo zimetoa taarifa ya pamoja na kulaani marufuku ya kuajiriwa katika idara za serikali wanawake wanaovaa hijabu na kuzuiliwa kuingia shuleni wanafunzi wanaojistiri kwa vazi hilo na kutaka kuweko uhuru kamili katika utumiaji wa vazi la hijabu.
Taasisi hizo 12 zisizo za kiserikali za Uturuki zimeeleza kuwa chama tawala cha nchini humo cha Uadilifu na Usawa kinachoongozwa na Waziri Mkuu Rajab Tayib Erdogan miaka kumi iliyopita kiliahidi kufuta marufuku hiyo ya hijabu na hivyo kuweza kujipatia kura nyingi za wananchi.
Taasisi hizo zimesema badala ya kuondoa marufuku hiyo dhidi ya hijabu chama tawala nchini Uturuki kinaonekana kupuuza takwa hilo kuu la raia wa nchi hiyo.
Licha ya serikali ya sasa ya serikali ya Uturuki kudai kwamba inafuata mafundisho ya Uislamu lakini viongozi wa nchi hiyo wangali wanatekeleza siasa za kupiga marufuku vazi la Kiislamu la hijabu katika shule na idara za umma.
Marufuku ya vazi la hijabu iliyoanza kutekelezwa nchini Uturuki 28 Februari mwaka 1997 inawasababishia matatizo mengi wanawake Waislamu nchini humo. 1094760
captcha