Hayo yamesemwa na hafidhi wa Qur'ani wa Sri Lanka Rahmatullah Sulaiman Ahmad ambaye anajitayarisha kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya nne ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu kutoka pembe mbalimbali duniani. Ameendela kwa kutoa mapendekezo ya kuboresha mashindano hayo akisema ni bora yafanyike kwa mzunguko katika nchi mbalimbali na kwamba aya anazopewa karii kusoma ziteuliwe kwa sadfa tu na si kupangwa na majaji hapo kabla.
Hafidhi huyo kutoka Sri Lanka amesema anasomea taaluma ya fizikia na hesabati katika chuo kikuu, ambazo hazina mfungamano wa moja kwa moja na Qur'ani Tukufu lakini kitabu cha Allah kina ishara za masuala ya kisayansi na kielimu.
Vilevile amezungumzia taathira kubwa ya Qur'ani Tukufu katika maisha yake na kuongeza kuwa Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu na kwa msingi huo hapana budi yana taathira kubwa na muhimu katika maisha ya mwanadamu anayeyahifadhi na kuyafanyia kazi.
Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu yatafanyika tarehe 12 hadi 15 Septemba katika mji wa Tabriz magharibi mwa Iran. 1070662