Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa makundi kadhaa ya Kimarekani yametangaza uungaji mkono wao kwa Wilders na kukitakia mafanikio chama cha mrengo wa kulia cha mbunge huyo anayepiga vita Uislamu cha Uholanzi katika uchaguzi unaofanyika kensho nchini humo.
Shirika hilo la habari limesema kuwa makundi hayo ya Kimarekani yamemuunga mkono Geert Wilders kwa kutumia kisingizio cha kupambana na kasi ya kuenea Uislamu katika nchi za Magharibi.
Moja ya makundi hayo ni Jumuiya ya Mashariki ya Kati ambayo inaunga mkono utawala katili wa Israel huko Philadelphia nchini Marekani ambayo pia iligharamia fedha za kesi za mwaka 2010 na 2011 za Wilders ambako alikabiliwa na tuhuma za kuchochea chuki dhidi ya Waislamu.
Jumuiya hiyo inawaunga mkono watu anaohujumu Uislamu na waandishi wanaoeneza chuki dhidi ya dini hiyo nchini Marekani kwa kutumia kisingizio cha uhuru wa kusema.
David Horowitz, mmiliki na mhariri mkuu wa jarida la Times of Israel ambalo ni maarufu kwa kuhujumu Uislamu ni miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Wilders. Anasema kuwa amempa mwanasiasa huyo fedha kwa ajili ya kutoa hotuba mbili zinazohujumu Uislamu huko Los Angeles na Philadelphia.
Mwanasiasa huyo mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akihujumu Uislamu na matukufu yake ikiwa ni pamoja na kutayarisha filamu ya Fitna inayovunjia heshima Qur’ani Tukufu na matukufu ya Kiislamu. 1096368