IQNA

Dakta Larijani: Ahlul Bait ndio marejeo ya kuielewa vyema Qur'ani Tukufu

17:07 - September 12, 2012
Habari ID: 2410255
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu yameanza leo mjini Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran.
Mashindano hayo ya kimataifa ya duru ya 4 yanawashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu na yanajumuisha hifdhi na kiraa.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu yanazishirikisha jumla ya nchi 52. Akihutubia katika ufunguzi wa mashindano hayo ya kimataifa ya hifdhi na kusoma Qur'ani kwa wanachuo wa ulimwengu wa Kiislamu, Dakta Ali Larijani Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa, saada ya dunia na akhera ya mwanadamu imo katika kuifahamu na kuidiriki Qur'ani Tukufu na kwamba, inawezekana kufahamu maarifa ya Qur'ani kupitia kushikamana kikamilifu na Watu wa Nyumba ya Bwana Mtume (rehma na amani ziwe juu yake pamoja na dhuria wake).
Spika wa Bunge la Iran amesema jamii ambazo zimetupilia mbali Qur'ani zimekosa pia uongofu. Amesema Qur'ani ina siri ambazo wanaozielewa vyema ndio wanaopata mafanikio ya kukielewa vyema kitabu hicho cha Allah.
Dakta Larijani amesisitiza kuwa kuna njia nyingi za kuweza kufahamu mafundisho na kina ya Qur'ani kulingana na uwezo wa kila mtu. Ameosema Mtume (saw) ametuamuru kurejea kwa Watu wa Nyumba yake ili kuweza kuelewa na kudiri kwa undani maana ya Qur'ani Tukufu.
Spika Larijani amesisitiza kuwa njia bora zaidi ya kuelewa Qur'ani Tukufu ni kurejea kwa Ahlul Bait (as) na hadithi zilizopokewa kutoka kwao. 1096829

captcha