IQNA

Wamisri waandamana kulaani filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw)

17:40 - September 12, 2012
Habari ID: 2410267
Maelfu ya raia wa Misri wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo wakilaani filamu iliyotengenezwa nchini Marekani ikimvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Maandamano hayo yamejumuisha watu wa makundi mbalimbali ya jamii ya Misri wakiwemo Wakristo na vyama mbalimbali vya kisiasa.
Waandamanaji hao wamelaani vikali filamu hiyo inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) ambayo imetengezwa nchini Marekani kwa ushirikiano wa mbunge anayepiga vita Uislamu wa Uholanzi Geert Wilders.
Jumuiya za Kiislamu na Kikristo za Misri zimetoa tarifa zikilaani vikali filamu hiyo. Waandamanaji hao pia wamepanga kufanya maandamano mengine makubwa mbele ya ubalozi wa Uholanzi mjini Cairo katika siku zijazo. 1096600


captcha